MWANAMKE AUAWA KIKATILI GEITA.
Bi,Esther Masangija mwenye umri wa maiaka 30 mkazi wa mtaa wa Mwatulole
kata ya Buhalahala mkoani Geita , ameuawa kwa kukatwa na mapanga sehemu mbali
mbali za mwili wake, huku mume wake ndele simon miaka 39 akijeruhiwa vibaya sehemu za
mwili wake hali ambayo imepelekea kulazwa katika hospitali teule ya rufaa mkoani hapa.
Esther
, aliuwawa baada ya kuvamiwa nyumbani
kwake na watu wasiojulikana majira ya saa nane usiku wa kuamkia febuari 18, ambapo marehemu ameacha mume na watoto 2 akiwemo wa mwezi 1.
wakizungumza
na PAUL BAHEBE BLOG mashuhuda wamesema kuwa
wavamizi waliotenda kitendo hicho walipitia dirishani na kuvunja kisha kuingia ndani na kufanikiwa
kutekeleza unyama huo.
Viongozi wa serikali ya mtaa na kata Mathias Mlasa ambae ni mtendaji wa kata hiyo na
diwani wa kata hiyo Mussa Kabese pamoja na mwenyekiti Charles Fikiri wamelaani vikali mauaji hayo na kuahidi
kuwa wote watakaobainika kuficha wahalifu
watapambana nao, kwani vitendo hivyo havivumiliki.
Kaimu
kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, Isaac Msengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na
kwamba taarifa za awali za chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro kati ya marehemu na mtu mmoja
ambaye jina lake limehifadhiwa na anashikiliwa
na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.
Bonyeza link hapo chini kuwasikia mashuhuda pamoja na viongozi wa mtaa huo wakizungumza;
http://www.audiomack.com/song/paul-bahebe-fm/mauaji-geita
Bonyeza link hapo chini kuwasikia mashuhuda pamoja na viongozi wa mtaa huo wakizungumza;
http://www.audiomack.com/song/paul-bahebe-fm/mauaji-geita
HABARI:JOEL MADUKA #Stormfm #Geita
Post a Comment