Header Ads

Polisi yawasaka wahariri Mawio


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawasaka wahariri na mmiliki wa gazeti la Mawio kutokana na habari mbalimbali ambazo wamekuwa wakichapisha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alisema jana kuwa wahariri hao wanatafutwa kwa ajili ya kusaidia uchunguzi unaofanyika kuhusu habari walizokuwa wakiziandika.

Sirro alisema wamekuwa wakiandika na kuchapisha habari ambazo zina utata, hivyo wanatafutwa kwa ajili ya kuthibitisha ukweli wake.alisema Siro.

Mbali na kusakwa kwa wahariri hao, jana kwenye mitandao ya kijamii, ilisambaa taarifa iliyoonekana kama tangazo la Serikali ya kulifungia maisha gazeti hilo bila kueleza sababu za hatua hiyo, ingawa halikuwa na saini ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye aliyetajwa kuandaa tangazo hilo.Nape alipotafutwa na Mwananchi kwa simu kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa ujumbe mfupi, “samahani, nipo kikaoni tuma msg!” Hata alipotumiwa ujumbe huo hakujibu.

Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyepatikana jana kuzunguzia taarifa hiyo.

Hata hivyo, baadaye usiku, Idara ya Habari (Maelezo), ilitoa taarifa kuwa Waziri Nape atazungumza na waandishi wa habari leo saa sita mchana, lakini haikueleza katika mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa idara hiyo atazungumzia nini.

Kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, Waziri wa Habari anaweza kulifungia gazeti wakati wowote akijiridhisha kwamba halikuendana na masilahi ya umma. Sheria hiyo imekuwa ikipingwa kwa maelezo kuwa imepitwa na wakati na inakandamiza uhuru wa habari     

No comments