Header Ads

YANGA YAMKABIDHI JEZI GARBA TAYARI KUANZA KAZI.

Bubakar
Klabu ya Yanga leo imemtambulisha rasmi mchezaji wao wa kimataifa kutoka Niger Issoufou Boubacar Garba baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga kuanzia sasa.
Garba amesajiliwa siku chache kabla ya dirisha dogo kufungwa baada ya benchi la ufundi la Yanga kujiridhisha na kiwango chake kufuatia majaribio ya muda mfupi aliyofanya kwenye kikosi hicho  chini ya kocha mkuu Hans van Pluijm.
Bubakar 1
Garba amesema kila kitu kinakwenda sawa na amewaahidi mashabiki wa Yanga kwamba, atapambana kuhakikisha anafanya vizuri na kuisaidia Yanga kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.
“Najisikia furaha tangu nimefika Tanzania kujiunga na Yanga, kila kitu kinakwenda sawa kuanzia kwa kocha, wacheaji pamoja na mashabiki. Yanga ni timu kubwa najivunia kucheza hapa na nawaomba mashabiki wasubiri kuona kutoka kwangu”, amesema Garba.
Bubakar 2
Amepewa jezi namba 14 ambayo kabla yake ilikuwa inavaliwa na beki wa kulia Joseph Zutta aliyesajiliwa kutoka Ghana lakini mkataba wake na klabu hiyo ulivunjwa kwa kile kilichodaiwa ni kushindwa kuonesha kiwango kilichotarajiwa na benchi la ufundi.
Mchezaji mwingine ambaye amesajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ni Paul Nonga ambaye hakuwepo wakati wa utambulisho kutokana na kurejea kwenye klabu yake ya amani ya Mwadui FC ya Shinyanga kwa ajili ya kuagana na timu hiyo na kufanya taratibu za kuhamia jijini Dar es Salaam.
Bubakar 3


No comments