Header Ads

Wakati Wa kubadilisha Maisha Yako Ni Sasa, Acha Kusubiri Tena.

Katika siku yetu ya leo ningependa nianze kwa kukuuliza swali hili, ni muda upi ambao unataka kubadilisha maisha yako kabisa?Inawezekana kuna wakati unaweza ukawa unajidanganya nakusema nitafanya hiki ama kile kesho au baada ya muda fulani na huku ukiendelea kusubiri na kufikiri huo ndiyo muda sahihi kwako. Ikiwa uko hivyo, ninachotaka kukwambia unajidanganya na unaendelea sana kupoteza muda wako kwa kusubiri huko.

Kama ulikuwa ukifikiri maisha yanakusuburi, naomba leo ubadili mtazamo wako mara moja na kujua kuwa maisha yako yanakutaka usonge mbele zaidi ya hapo ulipo sasa. Ni wakati wa kujitoa mhanga na kufanya mambo yote yaliyo muhimu ya kuweza kutimiza mipango na malengo yako uliyojiwekea katika maisha yako.

Huu si wakati wakutulia kusubiria mambo fulani yakutokee, ni wakati wa kusukuma kwa nguvu zote mpaka mafanikio unayoyahitaji yatokee. Sasa umefika wakati wa kuachana kung’ang’ania yale mambo yote yanayokukwamisha na kukurudisha nyuma na kuendelea mbele bila kuzuiliwa na kitu chochote kile.

Wakati ulionao sasa ni wakati wa kuibadilisha duniani uliyonayo na kuishi dunia mpya ya mafanikio. Jaribu kufikiri ndoto zako nzuri ulizokuwa ukizifiri kwa muda mrefu. Je unavyoona utazitimiza lini? Acha kuumiza na kusumbua kichwa sana, wakati wa kutimiza ndoto na mipango yako ni sasa ila tu kwa kuamua kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua.

Kwa kuwa bado una ndoto, muda, nguvu na dira nafasi ya kufanikiwa mpaka hapo sasa unayo tena kubwa hata kama unaona mambo yako yameenda vibaya sana. Acha kujiwekea visingizio vingi na kulalamika kusikokwisha hayo yote hayawezi kukusaidia badala yake chukua hatua zinazostahili kuweza kubadilisha maisha yako kwa nguvu zote.

Mpaka hapo tayari upo nyuma kimafanikio. Kama unafikiri natania jaribu kuangalia wenzako wako wapi sasa. Pia je jiulize hayo maisha uliyonao unastahili kuwa nayo ama umeyapata kutokana na kushikilia makosa ambyo yanakukwamisha sana kila siku. Acha kujitetea kwa lolote huo ndiyo ukweli unaotakiwa kuujua hata kama ukikuumia lakini mabadiliko kwako yanahitajika tena ya nguvu.

Ishi maisha yako yako sasa ukiwa kama unayetafuta ushindi. Acha kuishi maisha ya hofu ambayo yanakufanya ushindwe kuchukua hatua sahihi za kuweza hata kujitoa mhanga ili kutimiza ndoto zako. Jitoe, jitoe, nasema jitoe ili kuhakikisha ndoto zako zinatumia kwa namna yoyote na kuwa tayri kulipia gharama hizo muhimu.

Muda sasa ulionao ni wa kufanya kazi kwa bidii, kujituma zaidi na kuhakikisha unayapata maisha unayoyata kuwa nayo. Haiwezekani wengine wawe ndiyo wenye mafanikio halafu wewe ukashindwa kuyafikia. Uwezo wa kubadilsha maisha yao unao  ikiwa hilo utalichukulia kwa umakini wa hali juu.

Unaweza ukajiuliza sasa unaanzia wapi hiyo ni rahisi sana. Kuanzia leo jiwekee kiapo cha kuwa sasa mimi nimeamua kubadili maisha yangu kabisa na sitasubiri chochote na nitaanza na vile nilivyonavyo. Ukishafanya hivyo kisha chukua jukumu zima la kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA huko utakutana na familia nzima ya WANAMAFANIKIO ambapo utapata nafasi ya kujifunza mengi kupitia watu waliofanikiwa.

No comments