RICHARD LUYANGO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI KARAGWE.
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya karagwe
mkoani Kagera,limeapishwa rasmi kwa ajili
ya kuanza kufanya kazi walizotumwa na wananchi ili
kuwaletea maendeleo.
Akiwaapisha madiwani hao,hakimu mfawidhi wa
wilaya ya karagwe Paulo Faustine, amesema kuwa madiwani
wote wafanye kazi ya wananchi waliyowatuma na waache siasa za chuki
ambazo zinaweza kuvunja amani ya watanzania.
Faustine amesema kuwa madiwani wote walioapishwa hawana
budi kufuata sheria,kanuni na taratibu za
kutokuvunja kiapo
walichoapa bali wawatumikie wananchi na kuhakikisha
wanafanya siasa yenye amani ,busara na kudumisha amani ya nchi.
Vile vile mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
hiyo mhandisi Richard Luyango
amemtangaza mwenyekiti wa halmashauri hiyo Wales
Mashanda na makamu mwenyekiti Dausoni
Paul baada ya wote kuchaguliwa na kushinda kwa
kura 21 sawa na 70% kati
ya kura 30 zote zilizopigwa.
Hata hivyo mhandisi Luyango
amewataka madiwani wote bila kujali chama chochote kuwa na ushirikiano
katika kupanga mikakati ya kuleta maendeleo
katika wilaya ya Karagwe kwani siasa zimeisha na
kilichobaki ni kufanya kazi tu.
Post a Comment