Header Ads

RICHARD LUYANGO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI KARAGWE.

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya karagwe mkoani Kagera,limeapishwa rasmi kwa ajili ya kuanza kufanya kazi walizotumwa na wananchi ili kuwaletea maendeleo.

Akiwaapisha madiwani hao,hakimu mfawidhi wa wilaya ya karagwe Paulo Faustine, amesema kuwa madiwani wote wafanye kazi ya wananchi waliyowatuma na waache siasa za chuki ambazo zinaweza kuvunja amani ya watanzania.

Faustine amesema kuwa madiwani wote walioapishwa hawana budi kufuata sheria,kanuni na taratibu za   kutokuvunja kiapo walichoapa bali wawatumikie wananchi na kuhakikisha wanafanya siasa yenye amani ,busara na kudumisha amani ya nchi.

Vile vile  mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo mhandisi Richard    Luyango amemtangaza mwenyekiti wa halmashauri hiyo  Wales Mashanda na makamu mwenyekiti Dausoni Paul  baada ya wote kuchaguliwa na kushinda kwa kura 21 sawa na  70% kati ya kura 30 zote zilizopigwa.


Hata hivyo mhandisi  Luyango amewataka madiwani wote bila kujali chama chochote kuwa na ushirikiano katika kupanga mikakati ya kuleta maendeleo katika wilaya ya Karagwe kwani siasa zimeisha na kilichobaki ni kufanya kazi tu.

No comments