Header Ads

Rais Magufuli Awaongoza Watanzania Kufanya Usafi.



Leo Rais John Magufuli ameongoza Watanzania kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi, yuko eneo la ufukwe karibia na Ikulu akifanya usafi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye yuko kwenye soko la Kariakoo akiongoza wafanyabiashara wa soko hilo kufanya usafi.

Ni siku ya kihistoria kwa taifa tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwamba siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania watu huelekea viwanja vya Uhuru kuungana na wengine kuadhimisha siku hii ambapo leo ni miaka 54 tangu uhuru kupatikana,lakini  watu wanafanya usafi kuboresha mazingira ikielezwa ni UHURU na KAZI,ikienda sambamba na kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu

No comments