Mufti Mkuu wa Tanzania 'Atumbua Majipu' Mengine.
Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Alhaji Abubakari Zuberi ameivunja mamlaka ya uendeshaji na usimamizi wa msikiti mkuu wa mkoa wa Arusha na kuweka mamlaka mpya ili kuimarisha utendaji.
Akitangaza maamuzi hayo kwa niaba ya mufti Sheikh mkuu wa mkoa wa Arusha Shabani Juma alisema anaamini kuwa mamlaka mpya iliyowekwa itafanya kazi kwa ufanisi na kwa kasi ya hali ya juu pamoja na kujipanua ili kwafikia waumini wengi kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwahudumia kwa ukaribu.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa mamlaka iliyovunjwa wamesema kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo kwani hawakushirikishwa wakati wa vikao vya maamuzi vya mkoa vilivyojadili majina kumi na tano ya wajumbe yaliyotumwa kwa mufti kwa ajili ya uteuzi huo wa mamlaka mpya.
Kwa upande wao wajumbe wapya waliochaguliwa kuingia katika mamlaka hiyo mpya wamesema kuwa wanachangamoto kubwa ya kuwaunganisha waumini pamoja na viongozi wao ili kuleta maendeleo na kudumisha mshikamano.
Post a Comment