HALMASHAURI YA WILAYA GEITA YATUHUMIWA KWA WIZI.
Chama
cha mapinduzi ccm,mkoani Geita,kimemtaka mkurugenzi
wa wilaya ya Geita,kuchunguza na kuunda tume ya kufatilia ufisadi wa kiasi cha sh,milioni 300 kati ya sh,billion
1.2 zilizotolewa kwa ajili ya
ununuzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara.
Kauli
hiyo imetolewa na mwenyekiti wa ccm mkoani hapa,na
mbunge wa jimbo la Geita,Joseph Kasheku Msukuma,wakati
wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kilichofanyika
katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya geita.
Amemtaka
mkurugenzi kutokukubali kupokea mitambo bila ya kuwa na taarifa kamili ya vitu
ambavyo vimepungua katika mitambo hiyo.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya hiyo,Elisha Lupuga,
amekili kusaini mikataba ya kupokea mitambo hiyo bila ya kujua kuwa mitambo hiyo ilikuwa
chini ya kiwango.
Aidha
mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya,Ally Kidwaka,amesema
kuwa mitambo hiyo bado haijapokelewa na kwamba
ameunda tume ya watu wanne kuhakikisha wanafuatilia na kuchunguza
ubora wa mitambo hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya geita,Manzie Omary Manguchie,amewataka
madiwani hao kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu na kuachana na vitendo vya rushwa ambavyo
vimekuwa vikisababisha kushuka kwa maendeleo
katika wilaya hiyo.
Post a Comment