RAIS MAGUFULI HONGERA TUNAAMINI HIZI CHANGAMOTO UZITAZITATUA.
MGUSU
Ni kijiji
kilicho upande wa magharibi mwa mji wa Geita takribani kilometa 25 kutoka Geita
mjini.
Kilianza
mnamo Novemba 1987,shughuli kuu za kiuchumi katika kijiji hicho ni uchimbaji wa
madini.Mpaka sasa
kijiji hiki kina zaidi ya watu 12,000 ambapo tayari kimepewa hadhi ya kuwa kata
kutokana na wingi wa watu.Kijiji hiki
ni moja kati ya vijiji vyenye changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa
miundo mbinu muhimu kama barabara,afya,maji na Elimu. AFYAMpaka sasa
kijiji hiki hakina zahanati wala kituo cha afya hali inayopelekea baadhi ya
vifo vya kina mama wakati wa kujifungua kutokana na umbali wa huduma hiyo
muhimu ya afya ambapo watu hulazimika kusafiri umbali mrefu hadi Geita mjini
kuifuata.
ELIMUKatika
kijiji hiki pia kuna shule moja ya msingi ambayo ina zaidi ya watoto 1000,hata
hivyo shule hii inakabiriwa na changamoto lukuki ikiwa ni pamoja na ukosefu wa madawati,madarasa
machache ambapo ndani ya chumba kimoja cha darasa hulazimika kukaa watoto zaidi ya mia moja,changamoto nyingine ni pamoja
na walimu wachache,vitabu na zana nyingine za kufundishia.
Hali hii inawafanya
walimu walio katika shule hii kuwa na wakati mgumu sana katika kutekeleza
majukumu yao na kufanya kiwango cha elimu kuwa duni shuleni hapo.
Upande wa
shule ya sekondari nayo pia ipo moja(SHANTAMINE)
ambayo ni ya kata nayo hata hivyo ipo umbali wa zaidi ya kilometa 18 kutoka
kijijini hapo.Wanafunzi wanaosoma katika shule hii wanakabiriwa na wakati mgumu
kwani wengi wao huwawia vigumu kufika shuleni hapo kutokana na umbali uliopo
ambapo nauli kufika shuleni kwenda na kurudi ni shilingi 5000,wengi wao
wanatoka familia maskini ambapo wakati mwingine huomba msaada(lift) kwenye
malori ili kufika shuleni.
Hata hivyo
si wote wanaoanza kidato cha kwanza hufanikiwa kuhitimu masomo yao hasa watoto wa kike kwani wengi huishia kubeba
ujauzito na kujikuta ndoto zao kuishia njiani.
Mambo
mengine yanayokikabili kijiji hicho ni pamoja maji kutokuwa safi kwani maji
wanayotumia kwa kiasi kikubwa yamezungukwa na maeneo ya uchanjuaji wa dhahabu
kwa kutumia madini ya mecury( zebaki) ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Mjumbe wa
Serikali ya kijiji Bwana John Peter anasema wao kama serikali ya kijiji wafanya
jitihada za kuongea na uongozi wa Wilaya ili kutatua changamoto hizo ambapo
hata hivyo hakuna utekelezaji wowote mbali na ahadi.Anaiomba serikali ikitazame
kwa jicho la tatu kijiji hicho kilichozungukwa na madini lakini hali yake bado
ni mbaya sana.
IMEANDALIWA NA: Paul William (Geita)
Post a Comment