UKAWA WAWEKEWA NGUMU KUTUMIA UWANJA WAJANGWANI.
Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umesisitiza kuwa utazindua kampeni zake siku ya jumamosi ya tarehe 29 mwezi huu katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam licha ya mizengwe wanayowekewa na mansipaa ya ilala ya kuwanyima kutumia uwanja huo kwa sababu ya kuwa na matumizi mengine siku hiyo.
Akizungumza na wanahabari mapema jana jijini Dar es salaam mwenyekiti wa NCCR mageuzi ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika siku ya jumamosi kama ilivyopangwa japo manispaa ya ilala imewaandikia barua ya kuwa na matumizi mengine siku hiyo.
Mbatia alisema kuwa wamepeka maombi ya kutumia uwanja huo na wamejibiwa kuwa kuna watu wameshauchukua kwa ajili ya kazi nyingine ambapo walipojaribu kuuliza ni mtu gani ili wazungumze naye manispaa hiyo imegoma kumtaja na kusisitiza kuwa uwanja huo utakuwa ukitumika siku hiyo ya jumamosi.
Mbatia amesema kuwa kumekua na mbinu chafu ambazo zinatumiwa na serikali kupitia wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya za kuhujumu harakati za kampeni za umoja huo lakini wamejipanga kuhakikisha kuwa wanatetea haki yao na kuleta usawa katika kampeni hizo.
Akitolea mfano wa mgombea EDWARD LOWASA jana kunyimwa kuendelea na ziara yake ambayo juzi ilipangwa kufanyika katika baadhi ya hospitali kuzungumza na wagonjwa huku mgombea mwenza wa chama cha mapinduzi SAMIA SULUHU akiendelea na zoezi kama hilo mkoani kilimanjario jambo ambalo alisema kuwa ni rafu ya wazi ambayo kamwe hawawezi kuivumilia.
Akizungumzia swala la kampeni ya chama cha mapinduzi siku ya uzinduzi kufanyika hadi saa kumi na mbili na nusu kinyume na sheria za uchaguzi mbatia amesema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi imekuwa ikikaa kimya kwa kuwa kitendo hicho kilifanywa na chama tawala lakini kingefanyika na chama cha upinzani lazima wangepigwa mabomu jambo ambalo amedai kuwa ni kuendelea kuwajaza hasira watanzania ambao wengi sasa wamekuwa na kiu ya mabadiliko nchini.
Post a Comment