UGUMU WA MAISHA WAMPELEKEA KUTEKA MTOTO GEITA.
Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia Nasib Abdul (21) kwa kumteka mtoto wa miaka 2,na kumpeleka kusikojulikana huku akidai kupatiwa Tsh milioni 5 ili aweze kumwachia huru mtoto huyo.
Kwa upande wake mtuhumiwa Nasibu Abdul amesema kuwa sababu za kumteka mtoto huyo ni tamaa ya pesa ambapo pia amesema mama yake mzazi amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu hali iliyopelekea kijana huyo kuingiwa na mawazo hayo mabaya ili apate pesa ya kumhudumia mama yake.
kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo.
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha Ipalamasa akiwa na mtoto huyo.
Aidha kamanda Konyo amesema wakati wote wa tukio hilo mtuhumiwa alikuwa akiwasiliana na Baba wa mtoto huyo akimtaka amtumie shilingi milioni 5,vinginevyo angefanya jambo lolote kwa mtoto huyo la kumdhuru.
Mama wa mtoto akiwa na mtoto wake aliyekuwa ametekwa.
Baba yake na mtoto aliyekuwa ametekwa.
.Kamanda Konyo amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao na kuhakikisha wanawalinda pindi waondokapo au wawapo nyumbani.Habari,picha Na:JOEL MADUKA GEITA
Post a Comment