Header Ads

MSAMA ANAWA MIKONO KWA ROSE.

RoseMuhando.jpg

“HAWA mastaa hawa bwana! Wana matatizo sana, hivi inakuwaje mtu unamsaidia kwa mambo mengi, halafu badala ya kukushukuru anaamua kukulipa maneno makali? Yaani msaada wangu wote kwa Rose (Muhando), matokeo yake anatukana ukristo!” Ndivyo anavyoanza kueleza kwa sauti iliyojaa uchungu, meneja wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando, Alex Msama.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Msama alionesha kusikitishwa na madai ya Rose aliyoyatoa akiwatuhumu waumini na wachungaji wa makanisa ya kikristo na baadhi ya wadau wa muziki wa Injili (akiwemo Msama), kuwa wanamtukana na kumfundisha ugaidi.
“Nimekuwa karibu na Rose kwa muda mrefu sana, namsaidia kwa mambo mengi, mimi si mtu wa kujivunia kumsaidia mtu, wala sitaki watu wajue nimemsaidia nini Rose, lakini natatua matatizo yake mengi mno, sasa kauli zake kwamba ameingia kwenye ukristo kufundishwa ugaidi, sijui eti kuna watu wanatumia kazi zake kujinufaisha, nimeumia sana.
“Kila anapokuwa anakumbana na matatizo na watu, iwe kafanya kweli au kasingiziwa, huwa natatua kwanza, nimetoka naye mbali sana, lakini kwa maneno hayo sioni tena haja ya kuendelea kujiweka karibu naye,” alisema Msama.

No comments