Header Ads

CHENGE Akanusha Kuhusika na Tuhuma za Escrow na Wala Hajawahi Kuwa na Mgongano wa Maslahi Kati ya IPTL na VIP.

TUME ya Maadili chini ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, leo katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar imezidi kumhoji, Mwanasheria Mkuu wa zamani, Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi anayemaliza muda wake anayetuhumiwa kupata mgawo wa fedha za Tegeta Escrow anazodaiwa kupata kutoka kwa mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineerung, James Rugemalira.

Awali Mwanasheria huyo alifikishwa mbele ya baraza hilo akidaiwa kukiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kupata mgawo wa fedha kutoka kwenye akaunti hiyo ambazo zinakadiriwa kuwa ni sh. bilioni 1.6.

Akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Jaji Hamis Msumi, Chenge alikanusha kuwa hahusiki na tuhuma za fedha za Escrow na wala hajawahi kuwa na mgongano wa maslahi kati ya IPTL na VIP.

Chenge alisema kuwa aliingia mkataba na Kampuni ya VIP katika kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya kampuni binafsi zilizowekeza IPL na kwamba hakuiingia mkataba wa makubaliano na kampuni hiyo ambayo iliingia mkataba na serikali.

Mambo yaliyoainishwa na shahidi wa upande wa serikali ni pamoja na kutumia wadhifa wake kama mtumishi wa umma kupata maslahi binafsi ambayo ni kinyume cha kifungu cha sheria, huku akidai kuwa Chenge amejihusisha na mngongano wa maslahi kutokana na uchunguzi uliofanyika katika vipindi mbalimbali akiwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Change akipangua hoja za mwanasheria wa serikali alisema kuwa serikali iliingia mktaba wa makubaliano ya kuzalisha umeme na Kampuni ya IPL wakati akiwa mwanasheria na baada ya kustaafu aliingia makubaliano ya mdomo na mmiliki wa VIP ya kutoa ushauri kuhusu masuala ya kitaalamu kwa IPL tu.

Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Mstaafu, Hamis Msumi aliahirisha kusikilizwa kwa shauri hilo kwa madai ya kuwa upande wa wanasheria wa serikali uende kuandaa taarifa iliyosahihi ili kumpelekea Chenge Agosti 11 kwa ajili ya kupitia na baadaye taarifa hizo kupelekwa kwa mwenyekiti wa tume Agosti 14 kwa ajili ya kutoa uamuzi sahihi

No comments