Header Ads

YANGA WATOA BARAKA KWA SHERMAN AENDE ZAKE SAUZ.

Image result for SHERMAN YANGAImage result for SHERMAN YANGA


Uongozi wa Yanga umetoa baraka kwa mshambuliaji wake, Kpah Sherman ambaye anatarajia kuondoka nchini kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afya katika moja ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo kabla ya kukamilisha usajili.


Sherman ameingia sokoni kutokana na uwezo wake kutolifurahisha benchi la ufundi la Yanga huku kukiwa na ushindani mkali wa namba ambapo washambuliaji wengine waliopo kikosini hapo ni Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Malimi Busungu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amesema kuwa, wapo katika mazungumzo ya mwisho na timu hiyo inayomhitaji Sherman.

“Dili lipo katika hatua za mwisho na pindi litakapokuwa sawa ataondoka nchini kwa ajili ya kufanya vipimo na endapo atafuzu basi atajiunga na timu hiyo ambayo siwezi kukutajia jina kwa sasa.

“Hatupendi aende huko halafu akapate tabu ila tunatata akacheze soka, ndiyo maana hatukutaka aende kwa ajili majaribio kwani hiyo siyo hadhi yake,” alisema Tiboroha.


Aidha, mtu wa karibu wa Sherman aliliambia gazeti hili kuwa, Sherman ataondoka keshokutwa Jumapili au Jumatatu kujiunga na timu ya Mpumalanga Black Aces.

No comments