Header Ads

UANDIKISHAJI BVR,KOMPYUTA YAIBIWA GEITA.

Image result for MASHINE ZA BVRImage result for MASHINE ZA BVR


Kompyuta ya kutunzia kumbukumbu za watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wilayani Nyang'hwale imeibiwa na watu wasiojulikana  katika kijiji cha Mabongo,kata ya Nyugwa mkoani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Ibrahim Marwa amethibitisha kuibiwa kwa kompyuta hiyo na kusema imetoweka katika mazingira ya kutatanisha.

Hata hivyo alisema polisi wilayani humo inawashikilian watu watano,akiwemo mwandikishaji mkuu na msaidizi wake.

Marwa alisema  tukio hilo lilitokea jumamosi iliyopita asubuhi wakati wakihamisha vifaa hivyo kutoka kwenye moja ya kituo katika kata hiyo kwa ajili ya kuendelea na kazi ya uandikishaji.
Alisema wakati waandikishaji  wanaanza kupanga mashine zao,ndipo walibaini kutokuwapo kwa mashine hiyo.



No comments