Header Ads

POLISI KAGERA YAUA MAJAMBAZI WANNE.


kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Augastine Leone Ollomi
Majambazi wanne waliokuwa wamejificha katika ziwa Buligi wilayani Karagwe kwa lengo la kutekeleza vitendo vya uharifu huku wakiwa na silaha mbalimbali za kivita wameuawa na jeshi la polis mkoani Kagera wakati wakijiandaa kuvamia na kupora mali za wananchi katika mapambano ya kujibizana risasi na jeshi hilo yaliyodumu kwa zaidi ya dakika tano .
Akiongea mara baada ya tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Augastine Leone Ollomi amesema jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema juu ya ujio wa majambazi hao ambao walikuwa wamejificha katika ziwa Buligi huku wakijiandaa kwenda kufanya matukio ya uharifu katika kijiji cha bisheshe wilayani Karagwe.
Amesema majambazi hao walianza kujibizana risasi na jeshi la polisi na kufanikiwa kuwaua majambazi wanne na hakuna askari yeyote aliyejeruhiwa.
Kamanda Ollomi ameongeza kwa kusema mkoa wa Kagera sasa unakabiriwa na matukio mbalimbali ikiwemo mauaji ya watu kukatwa koromeo na matukio ya majambazi ambayo yameanza kujirudia.
Ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Kagera kwa ujumla kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona viashiria vya watu wasio wema wanaoingia nchini na wanaopanga njama za kufanya matukio ya kiuharifu ili kwa pamoja waweze kudhibiti matukio hao yanayojitokeza mara kwa mara katika mkoa huo..


No comments