Header Ads

MWANACHAMA SIMBA AKIFIWA KULIPWA 250,000/-

KLABU ya Simba imefanya kweli tena baada ya leo kuzindua kadi mpya za uanachama ambazo zitatoa fursa kwa watakaojiunga kunufaika na bima ya maisha.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kadi hizo jijini Dar es Salaam leo mchana, Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, amesema kila mwanachama atakayejiunga na kuchukua kadi mpya, atapata bima ya maisha inayojulikana kwa jina la 'Simba Pamoja'.
Amesema bima hiyo itampatia mwanachama ambaye amelipa malipo yake ya mwaka ya uanachama fedha taslimu zisizopungua Sh. 250,000 ikiwa atapata msiba kwa kufiwa na mtoto, mke au yeye mwenyewe.
Aveva amesema malipo ya uanachama hayajabadilika na yanaendelea kuwa Sh. 1,000 kwa mwezi, hivyo mwanachama atalipa ada ya mwaka Sh. 12,000 kwa wanachama hai na Sh. 30,000 kwa wanachama wapya.
“Hii ndiyo klabu pekee Afrika Mashariki na Kati inayotoa fao hili kwa wanachama wake, Simba inajali sana wanachama wake na tutaendelea kuimarisha uhusiano wa klabu na wanachama,” amesema Aveva.MJENGWA

No comments