MAREKANI KUCHEZA FAINALI KOMBE LA DUNIA.
Marekani wanacheza fainali ya nne ya Kombe la Dunia kwa wanawake baada ya kuwafunga mabingwa mara mbili wa kombe hilo, Ujerumani katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Olmpic mjini Montreal.
Mshambuliaji wa Ujerumani Celia Sasic alikosa penalti katika dakika ya 58, lakini nahodha wa Marekani Carli Lloyd alifunga kwa njia ya kichwa dakika kumi baadaye.
Zikiwa zimebakia dakika sita mchezo kumalizika, Kelley O'Hara ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba aliifungia timu yake bao lililowahakikishia Marekani kucheza fainali baada ya kufunga akiwa karibu na lango la Ujerumani.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali Japan itapepetana na England Alhamis wiki hii. Na mshindi katika mechi hiyo atavaana na Marekani katika fainali itakayopigwa siku ya tarehe 6 Julai jijini Vancouver.BBC
Post a Comment