BURUNDI KUENDELEA NA RATIBA YA UCHAGUZI.
Waziri wa mambo ya ndani, Edouard Nduwimana, amesema ratiba ya uchaguzi haitabadilika.
Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadha kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania nafasi ya urais kwa mara ya tatu.
Viongozi wawili katika serikali ya Rais Nkurunziza - akiwemo mmoja wa makamu wa rais, Gervais Rufyikiri, na spika wa bunge la nchi hiyo, Pie Ntavyohanyuma, wamekimbilia Ubelgiji.
Wote wawili wamekuwa wakosoaji wa rais. Uchaguzi umepangwa kufanyika mwezi ujao. Uchaguzi wa wabunge unafanyika Jumatatu.
Post a Comment