Header Ads

SIMBA KUKABIDHIWA KOMBE TAIFA NA JPM



Na George Mganga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 2018.

Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia, amesema kuwa wamemwandikia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe yenye ombi la kumuhitaji Magufuli juu ya ugeni huo.

Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.

Mbali na Simba kukabidhiwa taji hilo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Magufuli atawakabidhi pia vijana wa Serengeti Boys Kombe la CEFACA chini ya miaka 17 walilolitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwa maba0 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Ngozi, jijini Bujumbura.

Sherehe za Simba na Serengeti Boys zitaanza majira ya saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.

No comments