Header Ads

WEMA NDIYO CHANZO CHA ZARI KUMWACHA MOND.

Zari aaninika kuwa tukio la Wema Sepetu na Diamond kukumbatiana kwa mahaba wakati wa sherehe ya kumkaribisha Maromboso au ‘Mbosso’ iliyofanyika mwezi uliopita katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam mbele ya hadhara ndicho chanzo cha kumwacha Baba Tiffa.
Akiongea katika kipindi cha runinga cha Dira ya Dunia ya BBC Swahili, Zari amesema, “Tulikuwa tunajaribu kuona we can move from hiyo sikendo ya kupata mtoto. So we can move forward lakini vitu kama hivyo leo unasikia hivi unaona vile sijui kukumbatiana huko na maex kwenye public vitu vya kunidhalilisha, kunifanya niwe very disrespect na watoto wangu unaona tu like it’s just not right.”

Zari ameongeza kuwa Diamond hakuwahi kumueleza chochote kuhusu picha hizo na wala yeye hakuwahi kumuuliza kwa kuwa aliona haina maana kwake.

No comments