Wizara ya Mambo ya Nje yatoa tamko Sakata la Madareva 24 waliotekwa DRC
Juni 29, 2017 madereva 24 wa malori wametekwa na kikundi cha waasi cha Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Akizungumzia tukio hilo Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashairiki, Mindi Kasiga, amesema kuwa madereva hao wametekwa wakiwa wanelekea katika mgodi wa dhahabu wa Namoyo katika jimbo la Mainiema unaomilikiwa na kampuni ya Banro Gold ya Canada.
Amesema kati ya madereva 24 waliotekwa, 21 ni Watanzania na 3 ni Wakenya hivyo Serikali inafanya jitihada za kuwaokoa madevera hao.
Mindi amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini DRC, madereva hao wametekwa na waasi wa kikundi cha Mai Mai, kilishambulia msafara wa malori hayo uliokuwa ukisindikizwa na askari wa jeshi la DRC (FARDC) na kufanikiwa kupora mali zao zote zikiwemo fedha na kuharibu malori hayo.
Amesema hadi sasa Serikali kupitia Ubalozi wake nchini DRC umechukua hatua kadhaa kuhakikisha madereva hao wanapatikana na wakiwa salama.
==>Hatua hizo ni;
1.Kuwasilisha rasmi tukio hili kwa serikali ya DRC na kuwaomba wasaidie kuwapata hawa watanzania.
2.Tumeomba Oparesheni inayoendelea dhidi ya waasi huko DRC itambue uwepo wa raia wa tanzania msituni ili wawasaidie haraka
3. Mawasiliano na madereva yanafanyika kujua hali zao
4.Mgodi wa Banro umetoa ushirikiano mkubwa ikiwemo kuwahamisha kwa muda wafanyakazi wa mgodi huo ikiwemo watanzania had hali itulie
5. Ubalozi unafatilia maombi ya kukutana na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo ili kuomba wasaidie madereva hao wapatikane salama
Post a Comment