Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi
Bondia maarufu nchini Tanzania Francis Cheka, jana ametangaza rasmi kustaafu mchezo wa msumbwi kwa kile alichokieleza ni ubabaishaji wa ma-promota pamoja na kutopata faida katika mchezo huo.
Cheka ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuchukua pesa na kugoma kupanda ulingoni katika pambano lililokuwa limeandaliwa siku ya Krismasi, amesema amechoshwa na kile alichokiita kuwa ni utapeli wa mapromota, na kwamba sasa atajikita zaidi katika mapambano ya kuhamasisha vijana.
Akiwa amedumu kwenye ngumi nchini kwa takribani miaka 19, Cheka amesema mchezo huo umetawaliwa na majungu, na fitina huku watu wengi wakifikiri kuwa kuna pesa nyingi, wakati hakuna anachokipata zaidi ya umaarufu na kuhojiwa kwenye vyombo vya habari.
"Huu mchezo una majungu na fitina, hakuna faida yoyote zaidi ya kuhojiwa na waandishi wa habari, hakuna pesa, tunapata pesa gani, watu wanadhani tunapata pesa, nitabaki kucheza mapambano kwa ajili ya kuhamasisha vijana katika ngumi pamoja na kufanya biashara nyingine nipate pesa, nimedumu kwenye ngumi zaidi ya miaka 19, nimevumilia mengi" Alisema Cheka.
Post a Comment