SARE ZA CCM ZADAIWA KUMSHUSHA CHEO MKUU WA SHULE KASAMWA.
Picha:kwa msaada wa mtandao(haihusiani na tukio)
Miongoni mwa stori kubwa katika magazeti ya leo Tanzania zilizoshika mitandao ni pamoja na ile ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kasamwa mkoani Geita, Dennis Otieno kudaiwa kushushwa cheo kutokana na kuzuia wanafunzi kuvaa sare za CCM kwenye mahafali ya kidato cha nne.Habari hiyo iliyopewa uzito wa juu katika gazeti la Mwananchi ambapo inasomeka "KLABU YA JPM YAMSHUSHA CHEO MKUU WA SHULE".
Taarifa hizo zinasema mkuu huyo wa shule alipinga kitendo cha baadhi ya walimu kuchangisha fedha wazazi wa watoto ambao ni wanachama wa Klabu ya Magufuli ili kufanya sherehe hilo kutokana na agizo la Rais la kufuta michango yote mashuleni.
Otieno, ambaye alikataa kuzungumzia suala hilo, anadaiwa kushushwa cheo kutokana na shinikizo la makada wa chama hicho tawala, hasa mwenyekiti wa CCM mkoani Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, ambaye amethibitisha kushushwa cheo kwa mtumishi huyo wa umma.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinasema Otieno aligombana na mwalimu ambaye ni mlezi wa Klabu ya Magufuli kutokana na kuandaa mahafali hayo.
Post a Comment