MWENYEKITI WA CHAMA CHA WATU WENYE UALIBINO MKOANI MWANZA ALIA NA VYOMBO VYA HABARI.
Picha kutoka Maktaba, Mwenyekiti TAS akizungumza Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye Ualibino mkoani Mwanza, Alfred Kapole, amevitaka vyombo vya habari kuendelea kukemea matukio ya unyanyasaji, utekaji na mauaji kwa watu wenye ualibino nchini ili kusaidia kutokomeza vitendo hivyo.
Kapole ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm juu ya mchango wa vyombo habari katika kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini ambapo amebainisha kwamba bado mchango wa vyombo vya habari kuripoti matukio hayo hauridhishi ikilinganishwa na matukio mengine.
Kapole ameongeza kwamba ni vyema washukiwa wa vitendo vya utekaji na mauaji ya watu wenye ualibino wakachukuliwa hatua kali za kisheria jambo ambalo litasaidia vitendo hivyo kutokomezwa.
Amebainisha kwamba kati ya kesi 27 zinazohusisha utekaji na mauaji ya watu wenye ualibino mkoani Mwanza, ni kesi tatu pekee zilizokwishatolewa maamuzi mahakamani huku kesi nyingine zikichukua muda mrefu kutolea maamuzi jambo ambalo linakwamisha mapambano dhidi vitendo hivyo.
Post a Comment