Wazawa wa mkoa wa Kagera washauriwa kuguswa na madhara ya tetemeko la ardhi.
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum mstapha Kijuu amewashauri wazawa
wa mkoa wa Kagera wanaoishi katika maeneo mbalimbali yaliyoko hapa nchini na
nje ya nchi wenye uwezo kiuchumi kuguswa na athari iliyowakumba wananchi
wanaoishi katika mkoa huo iliyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
humo kusababisha madhara makubwa ambayo ni pamoja na uharibifu mkubwa wa nyumba
za makazi pamoja na vifo vya watu 17.
Mkuu
huyo wa mkoa ametoa ushauri huo kwa nyakati tofauti wakati akipokea misaada
mbalimbali ya kibinadamu inayoendelea kutolewa na makampuni, taasisi za
kiserikali na zile za binafsi, amesema mwikitiko wa wazawa wa mkoa huo katika
kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa tetemeko la ardhi hauridhishi
ukilinganisha na uwezo walionao kiuchumi baadhi ya wazawa wa mkoa huo.
Kauli
ya mkuu wa mkoa wa Kagera imeungwa mkono na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini
Wilfred Lwakatare ambaye amewahimiza wananchi katika mkoa wa Kagera kuwa kitu
kimoja katika kukabiliana na janga hili.
Mkuu
wa mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu Salumu mstapha Kijuu ameendelea kupokea
misaada mbalimbali ya kibinadamu toka kwenye taasisi binafsi, makampuni na
mashirika, misaada aliyoipokea leo ni ile iliyotolewa na kampuni ya Maurel et
Prom iliyotoa shilingi milioni 20, umoja wa wafugaji uliotoa mifuko ya saruji
400 na shirika la Kolping lililotoa mahema 100, baadhi ya wawakilishi wa
taasisi mashirika yaliyotoa misaada wanaeleza walivyoguswa na athari za
tetemeko hilo.
Post a Comment