TMA yatoa tahadhari tano kupungua kwa mvua nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dk Agnes Kijazi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa ,Dk Kijazi alisema vipindi vigumu vinatarajiwa kusababisha uvyevu unyevu mdogo hatua itakayoathiri ustawi wa mazao ya kilimo, mito na mabwawa kupungua maji yake kutoka hali iliyopo kwa sasa na mlipuko wa magonjwa kutokana na uhaba wa maji.
“Athari nyingine ni mafuriko yatakayojitokeza kupitia mvua kubwa zitakazotokea kwenye maeneo yasiyokuwa na uoto mwingi, pia kutakuwa na uhaba wa malisho ya mifugo ya wanyama katika maeneo mengi, hatua hiyo ya kupungua kwa mvua inatokana na kupungua kwa joto katika maeneo ya Bahari ya Pasifiki,”alisema.
Post a Comment