Serikali ya Kenya yakabidhi msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.
Serikali
ya nchi ya Kenya imekabidhi msaada wa hisani kwa waathirika wa tetemeko la
ardhi lililotokea katika mkoani Kagera na kusababisha madhara makubwa ambayo ni
pamoja na vifo.
Msaada
uliotolewa na serikali hiyo ni pamoja na mabati bando 4,000, magodoro 100 na
mablanketi 400 ambavyo kwa pamoja vimekabidhiwa na balozi wa Kenya nchini
Tanzania Chirau Ali Mwakwere kwa mkuu wa mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu
Salum Mstapha Kijuu, akizungumza baada ya kukabidhi msaada amesema nchi hiyo
imeguswa na madhara ya tetemeko pia imetoa msaada huo kwa kuzingatia mahusiano
mazuri baina ya nchi hizo mbili.
Kwa
upande wake, mkuu wa mkoa wa Kagera, meja jenerali mstaafu Salum Mstapha Kijuu
ameshukuru msaada uliotolewa na nchi hiyo na kueleza kuwa misaada zaidi bado inahitajika
kwa kuwa madhara ya tetemeko ni makubwa, naye waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu sera, bunge, ajira na walemavu, Jenista Mhagama amemueleza balozi huyo
hatua mbalimbali ambazo zimeishachukuliwa na serikali baada ya kutokea kwa
tetemeko hilo.
Post a Comment