MKUU WA WILAYA YA GEITA AAMURU VIONGOZI WA CHUO CHA UALIMU KUKAMATWA KWA KUSHINDWA KURUDISHA FEDHA
Mkuu wa wilaya ya Geita Mh.Herman Kapufi
Viongozi
hao wameamuriwa kukamatwa baada ya kushindwa kuwarejeshea wanachuo fedha
wanazodai kiasi cha shilingi milioni 230.
Hatua ya Kaimu Mkuu wa Mkoa huyo ambaye pia ni
mkuu wa wilaya ya Geita kutoa agizo hilo baada ya chuo hicho kudaiwa
kuwadaahili wanachuo wapatao 300 katika kozi ya Early Childhood Development
Education (ECDE) kozi ambayo haitambuliki na NACTE.
DC kapufi amesema kwa kipindi chote wanachuo walichokaa chuoni
hapo na kupotezewa muda wao ni lazima uongozi uwarudishie fedha zao pamoja na kuwapatia
vyeti.
Awali Kaimu Mkurugezi wa chuo hicho aliomba kulipa kiasi cha
shilingi milioni 115 kati ya fedha hizo jambo ambalo lilikataliwa na wanachuo
pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa.
Sakata hilo limeanza mapema mwezi huu baada ya wanachuo hao
kugoma kuingia madarasani wakishinikiza uongozi ulipe fedha zao wanazodai
ingawa kumekuwepo na mvutano mkali baina ya mkurugenzi wa chuo na aliyekuwa
mkuu wa chuo hicho.
Mkuu wa chuo anatuhumiwa kupokea ada na kuwadahili baadhi ya
wanachuo bila mmiliki wa chuo hicho Bwana Richard Mchele kushirikishwa kutambua
kuwepo kwa udahili wa wanafunzi wasio na sifa ulikuwa ukiendelea huku mmiliki
akiwa hajui chochote.
Post a Comment