Mkuu wa mkoa Mwanza aongoza Majeshi ya ulinzi na usalama kufanya mazoezi.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza, ambaye pia ni Mkuu wa mkoa huo John Mongella leo Alfajiri ameongoza majeshi ya ulinzi na usalama katika mkoa huo kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ambayo lengo lake ni kuwajenga askari kuwa wakakamavu na wenye nidhamu katika ulinzi wa taifa.
Vikosi vya majeshi vilivyoshiriki katika mazoezi ya kutembea yaliyoanzia uwanja wa furahisha na kupita mitaa mbalimbali jijini hapa,sambamba na kukimbia mchakamchaka na kisha kumalizikia tena katika uwanja huo kwa askari,maofisa na mkuu wa mkoa kufanya mazoezi ya viungo ni jeshi la ulinzi la wananchi tanzania ( JWTZ ),polisi,magereza,uhamiaji,zimamoto na uokoaji na mgambo.
Baadhi ya askari wa vikosi mbalimbali vya majeshi wakizungumza baada ya mazoezi ya pamoja kuhitimishwa na mkuu wa mkoa John Mongella katika uwanja wa furahisha,wamefurahishwa na mazoezi hayo na kuomba yawe endelevu ili kuwajenga kiafya na kuwafanya wawe wakakamavu na jasiri katika kupambana na vitendo mbalimbali vya uhalifu nchini.
Post a Comment