Header Ads

Mauaji ndani ya Mgodi wa GGM: ni baada ya kuingia mgodini kinyume na utaratibu

KIJANA mmoja Chacha Gailingi (30) mkazi wa Nyankumbu wilaya na Mkoa wa Geita amefariki dunia huku mwenzake Nelson Busumabu(18) akidaiwa kuteguka kiuno baada ya walinzi wa mgodi kuchimba dhahabu  GGM kuwashushia kichapo na kuwatumbukiza kwenye shimo la maji kwa kile kinachodaiwa kuingia mgodini kinyume na utaratibu.
Tukio hilo lililoacha simanzi kubwa kwa wakazi wa mji wa Geita , limetokea Tarehe 20 mwezi huu majira ya saa 11 jioni  katika Mgodi wa GGM ambapo vijana hao inadaiwa waliingia kwa ajili ya kuokota mawe ya dhahabu.
Wakizungumza na channel Ten nje ya ofisi za mkuu wa wilaya ya Geita walikofika kuomba msaada , ndugu na jamaa wa watu hao wamesema kitendo kilichofanywa na walinzi wa GGM si cha kiungwana na kuwaomba waliofanya hivyo kuchukuliwa hatua kali.
Akizungumza kwa shida huku akiwa amelala katika ofisi hizo , Nelson Busumabu ameeleza jinsi walivyofanyiwa na walinzi huku akililalamikia  jeshi la polisi kumnyima pf3 kwenda kutibiwa.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Mponjoli mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake.
CHANZO:CHANEL TEN

No comments