Header Ads

Darasa la saba kuanza mitihani kesho

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza rasmi kuanza kwa Mtihani waa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), utakaofanyika Septemba 7 na 8, mwaka huu, kote nchini.

Akitoa taarifa kuhusu mtihani huo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 795,761 katika shule 16,350.

Dk Msonde ametoa wito kwa walimu na wanafunzi kuwa waaminifu kwenye mtihani huku akizitaka jamii zinazozungunga maeneo ya shule hizo kuwa watulivu katika kipindi ambacho wanafunzi wanafanya mitihani yao.

“Baraza halitasita kuchukua hatua kwa mtu yoyote atakayehusika na udanganyifu katika  mitihani,”amesema Dk Msonde.

No comments