Kama wewe ni mwoga wa kupanda sehemu zenye kimo kirefu kama maghorofa, minara, ngazi, miti au sehemu zenye muinuko, basi woga wako utaimarika na kuwa maradufu kama utapata nafasi ya kipekee ya kutembea kwenye njia ya glasi iliyopo kwenye ukingo wa mlima mmoja nchini China.
Mlima wa Tianmen uliopo katika Hifadhi ya Msitu wa Zhangjiajie katika jimbo la Hunan wenye urefu wa  takribani mita 1,403 kutoka katika usawa wa bahari  umechukua sura ya kipekee nchini China, baada ya kujengewa njia ama kijinjia cha kupitia watu kilichotengenezwa kwa glasi ambayo ina urefu wa takribani  mita 100 na upana wa mita moja nukta sita (1.6m).
glass-bridge-zhangjiajie-national-forest-park-tianmen-mountain-hunan-china-2
Mlima huo wenye jina maarufu la ‘Coiling Dragon Cliff skywalk’ ama hakika hauwafai wale ambao wana ugonjwa wa moyo na wenye kuzimia ovyo kwasababu ya hofu ya kimo ambacho kinatishia maisha, watu wenye ujasiri wanakaribishwa kupanda mlima huo na kutembea kwenye njia hiyo ya glasi ili kuweza kufaidi mandhari nzuri kutoka juu ya mlima huo wenye uzoefu wa aina yake.
Aidha hifadhi hiyo ya msitu wa Zhangjiajie ni makazi pia vijinjia vingine vitatu pamoja na daraja lenye urefu wa mita 430 ambalo pia limetengenezwa kwa glasi linaloning’inia mita 180 kutoka katika usawa wa ardhi
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)
glass-bridge-zhangjiajie-national-forest-park-tianmen-mountain-hunan-china-6
glass-bridge-zhangjiajie-national-forest-park-tianmen-mountain-hunan-china-10
glass-bridge-zhangjiajie-national-forest-park-tianmen-mountain-hunan-china-9
glass-bridge-zhangjiajie-national-forest-park-tianmen-mountain-hunan-china-12