MAUAJI UTURUKI: PAPA FRANSISI AWAOMBEA WAHANGA
Papa Fransisi amewaombea wahanga wa mlipuko wa bomu uliotokea kusini mwa Uturuki jumamosi. Takribani watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya dazani wamejeruhiwa wakati mtu anayeshukiwa kujitoa mhanga alipolipua bomu katikati ya watu kwenye harusi katika jiji la Gaziantep. Wanawake na watoto ni kati ya waliouawa.
Rais wa uturuki Tayyip Erdogan amesema inahisiwa kuwa kikundi cha Islamic State ndicho kilichohusika na shambulizi hilo.
Papa amesema “ Habari za huzuni zimenifikia zinazohusiana na shambulio baya” lililofanyika katika nchi pendwa Uturuki.” “ Tuwaombee wahanga, waliopoteza maisha na majeruhi, na tunaomba zawadi ya amani kwa wote.”
Post a Comment