Magufuli: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Pumzika Kwa Amani.......Wewe upo Salama, Usisikilize kelele za Nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kwamba serikali itawalinda wastaafu nchini wakiongozwa na viongozi wakuu wa umma ili wawe na heshma yao ndani ya jamii.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi.
''Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wewe pumzika kwa raha zako , upo salama watachonga wee lakini mimi kama Rais wa awamu ya tano nipo tayari kuwalinda watumishi wote wastaafu kwa kuthamini mchango wao ndani ya taifa hili''
Aidha Rais Magufuli amesisitiza kwamba uchaguzi nchini umemalizika hivyo vyama vyote vya siasa viongeze nguvu baada ya miaka mitano ili apimwe na wananchi waliomchagua kama ametekeleza ahadi zake.
''Niwaombe wanasiasa wenzangu uchaguzi umekwisha, kama ni wabunge jielekezeni bungeni, kama ni madiwani jielekezeni kwenye maeneo yenu, sitakubali mtu yeyote anikwamishe katika kutimiza ahadi zangu kwa wananchi'' Amesema Rais Magufuli.
Kuhusu tume ya uchaguzi kukabiliwa na changamoto lukuki Rais Dkt. Magufuli amesema fedha za tume hiyo ilizobakiza kiasi cha shilingi bilioni 12 na kuzirudisha serikalini, serikali imeruhusu fedha hizo zitumike kujenga jengo la tume hiyo ili kuondokana na gharama za kupangisha jengo wanalotumia kwa sasa.
Aidha akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa huru na wa haki na hata waangalizi wa nje wengi wamepongeza uchaguzi huo.
Post a Comment