Header Ads

Wabunge Wanawake wa UKAWA watoka nje ya Bunge baada ya Mbunge wa CCM Kuwatuhumu Kwamba Wamepata Ubunge Kwa Kufanya Mapenzi na Viongozi Wao

Wabunge wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga (CCM ) aliyedai jana kuwa viti maalum Ukawa hutolewa kwa rushwa ya ngono.

Mlinga alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia hotuba Wizara ya Katiba na Sheria  ambapo alisema ili uweze kuwa mbunge wa viti maalum chadema, lazima ufanye mapenzi na kiongozi wako wa chama.
 
Wabunge hao leo asubuhi  waliomba mwongozo kwa Naibu Spika 
kupitia kwa Mbunge Sophia Mwakagenda wa viti maalumu (Chadema)kumtaka mbunge huyo athibtishe kauli yake  lakini hawakusikilizwa na badala yake Naibu spika aliwataka wakae chini.

Baada ya mabishano ya dakika kadhaa pasi kusikilizwa, wabunge hao walisimama wote na kuamua kutoka nje  ya ukumbi wa bunge huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa.

Kusikiliza sauti bonyeza HAPA

No comments