Tume ya maendeleo ya ushirika yakusudia kuvifuta vyama 1,862 vilivyokiuka matakwa ya Sheria.
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Audax Peter Rutabanzibwa akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) Kuhusu makusudio ya Tume hiyo kuvifuta vyama 1862 katika daftari la vyama vya Ushirika vyama ambavyo vimekiuka matakwa ya sheria ya vyama vya ushirika No.6 ya mwaka 2013. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto Afisa Uhusiano wa Tume hiyo Bw. Bunyanzu Ntambi.
PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO
Tumeya Maendeleo ya Ushirikainakusudia kuvifuta katika Datari la Vyama vya Ushirika vyam a ambavyo vimekiuka matakwa ya Sheria ya Vyama vya UshirikaN a.6 ya mwaka 2013. Kwa mujibu wa sheria, Mrajis wa Vyama vya Ushirika, kwa mamlaka aliyopewa chini ya vifungu Namba 11(3), 8(2) na 100 anatakiwa kuvifuta vyama ambavyovimeshindwa kufa nya kazi katika kutimiza masha rti ya usajili wake. Masharti y aliyokiukwa ni pamoja na kutok ufanya Mikutano kwa mujibu wa Sheria, kutokufanya chaguzi za viongozi kwa mujibu wa Sheria , kuwa na idadi pungufu yawana chama na kushindwa kufanya shu ghuli zake kwa zaidi ya miezi sita, kinyume na matakwa ya Sh eria na masharti ya vyama hivy o. Kutokana na sababu hizo, vyamavinavyokusudiwa kufutwa ni 1862 na vitafutwabaada ya siku tisini (90) kuanzia tarehe 13 Mei, 2016 siku ambayo Tangazo la Ku sudio la Kufuta vyama hivyo il ipochapishwa katika gazeti la Serikali. Idadi ya vyama vinavyokusudiwakufutwa katika kila mkoa ni k amaifuatavyo: Arusha vyama 83, Dar es Salaam 91, Dodoma 50, Geita 16, Iringa 74, Kagera 240, Katavi 19, Kig oma 38, Manyara 73, Mara 203, Morogoro 278, Mtwara 52, Njombe 18, Pwani 324, Rukwa 14 , Ruvuma 14, Shinyanga 89, Simiyu 93, S ingida 15, Tanga 77 na Lindi 1 . Orodha ya vyamavinavyokusudi wa kufutwa inapatikana katika Ofisi za Ushirika za Wilaya na Mikoa na katika tovuti la Tume ya Maendeleo ya Ushirika(www. ushirika.go.tz ) . Mtu yeyote au Taasisi yenye pingamizi la msingi dhidi ya kuf utwa kwa chamahusika, anatakiw a awasilishe pingamizi hilo na sababu zake katika Ofisi ya M rajis kupitia Ofisi za Warajis Wasaidizi wa Mikoa husika ndan i ya siku tisini (90) kuanzia tarehe 13/05/2016, siku ambayo tangazo la kufutwa kwa vyama hivyo lilipotangazwa katika gaz eti la Serikali. Umma unataarifiwa kwamba zoezila kufuta Vyama vya Ushirika ambavyo haviendeshwi kwa mujibu wa Sheria ni endelevu na kwa ajili hiyo viongozi na wanacham a wa vyama vya Ushirika na Maa fisa Ushirika wanaagizwa kuhak ikisha kwamba Vyama vya Ushirik a katika maeneo yao viendeshwe kwa kuzingatia matakwa ya Sher ia ya Vyama vya Ushirika ili k uepuka vyama vyao kufutwa.
Post a Comment