Header Ads

Mpinzani mkuu wa Donald Trump John Kasich amejiengua.

Mpinzani mkuu wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha tiketi ya urais wa chama cha Republican , John Kasich amejiengua.
Gavana huyo wa jimbo la Ohio ametangaza kusitisha kampeini zake baada ya kura ya maoni kuonesha kuwa umaarufu wake hauwezi kumpiku Donald Trump kutwaa tiketi ya chama cha Republican kuwania urais wa Marekani.
Kujiondoa kwake kunakuja baada masaa 24 ambapo Seneta wa Texas Ted Cruz alitangaza kuachia ngazi, baada ya ushindi wa Donald Trump katika kura za mchujo zilizopigwa katika jimbo la Indiana Jumanne usiku.
Kufuatia hatua hiyo Bw Trump anapigiwa upatu kutawazwa kuwa mgombea wa chama cha  Republican.
Awali Mpinzani mweza ambaye ni Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz naye alijiondoa mapema wiki hii kufuatia kushindwa na Trump katika jimbo la Indiana .

No comments