UMOJA WA WAGANGA WA TIBA ASILIA MKOANI GEITA WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA NYANG'WALE
Umoja wa waganga wa tiba asili wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita umempongeza mkuu wa wilaya mh Ibrahim Marwa, kwa kutoa ushirikiano ambao umesaidia kupunguza kasi ya mauwaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi.
Akitoa taarifa hiyo katika mkutano wa waganga wa tiba asilia wilayani humo mwenyekiti wa umoja huo kanda ya ziwa Bujukano John Mahungu amesema kuwa ushirikiano uliokuwepo kati ya umoja huo na uongozi wa wilaya umefanikisha kupunguza mauaji kutoka asilimia 80% mwaka 2014 hadi kufikia 10% hivi sasa.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale mh Ibrahim Marwa ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika mkutano huo ,amesema kuwa kwa sasa wilaya yake imedhamiria kushirikiana na viongozi wa vijiji kukusanya takwimu za wazee ikiwa ni moja kati ya njia za kudhibiti wimbi la mauaji.
Aidha Marwa ameushukuru uongozi wa waganga wa tiba asilia kwa kutoa elimu kwa waganga waliotoka maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na ulinzi shirikishi hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mauaji katika maeneo yao.
Post a Comment