Header Ads

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) KUDHIBITI MAADILI YA UTANGAZAJI NCHINI.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imesema iko katika hatua za mwisho za uundaji wa kitengo maalum kitakachokuwa kikidhibiti maadili ya utangazaji nchini ili kuhakikisha maadili ya Mtanzania yanalindwa.

Adhima hiyo ya Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imetolewa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Maudhi ya TCRA,huku ikisisitiza lazima sheria za utangazaji zifuate ili kulinda maadili ya Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt Ally Simba amesema uwepo wa Kamati ya Maudhui ndani ya TCRA ni muhimu katika kuhakikisha wanadhibiti ukiukwaji wa sheria za utangazaji.

Kamati  hiyo ambayo ni ya Nne kuuundwa kwa nyakati tofauti inaongozwa na Prof, Haji Semboja, ambapo pamoja na masuala mengine imemhakikishia Waziri huyo wa Habari nchini kuwa itajitahidi kuhakikisha inaangalia namna ya uboreshaji wa tasnia ya habari nchini.

Awali Waziri huyo wa Habari alipata fursa ya kutembelea Makumbusho ya Mawasilinao ya TCRA ambayo imesheheni vifaa vya zamani vya utangazaji, kama vile  simu, luninga, radio, ambapo vifaa vya zamani vya utangazaji vya ITV, pia vimehifadhiwa ndani ya makumbusho hiyo.

CHANZO:88.9 STORMFM 

No comments