Header Ads

Hamphrey Polepole aukwaa U-DC Musoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza jana tarehe 19 Aprili, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016

No comments