Header Ads

GARI LA WAGONJWA LILIKATALIWA-LEMA.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema CHADEMA amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Mwivaro 'Ambulace' ambayo itakayosaidia wagonjwa katika eneo hilo ikiwa ni moja ya ahadi zake kwa wananchi.

Akizungumza na EATV Lema amesema gari hilo alilinunua tokea mwaka jana lakini alikuwa amelipaki kutokana na serikali kukataa kulipokea kwa hofu kwamba wangempa umaarufu wa kisiasa.

''Gari hili nililinunua mwaka jana lakini serikali wakakataa kulipokea nikalipaki na nikahimiza wananchi wa jimbo langu kunichagua ili tulete maendeleo ya kweli na baada ya kupata madiwani wa kutosha na Meya wa jiji sasa wananchi wategemee mambo makubwa zaidi katika jimbo langu na jiji kwa ujumla''-Amesisitiza Lema.

Aidha Mbunge huyo amesema kwa sasa anafanya kazi za maendeleo vizuri kwa kushirikiana na viongozi wa serikali na hakuna tatizo kubwa katika mahusiano ya viongozi wa serikali kama ilivyokuwa hapo awali.

No comments