WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KATIKA KATA YA LUDETE WILAYANI NA MKOANI GEITA.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa geita Mponjoli Lotson.
Watu wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa na wananchi katika kata ya Ludete wilayani na mkoani Geita kwa kile kinachosadikika kuhusika katika tukio la kujaribu kuvamia katika nyumba ya Bw.Deusi Francis mkazi wa kijiji cha Lwamgasa Mkoani hapa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Geita Bw.Mponjoli Lotson amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia machi 21 majira ya saa kumi usiku ambapo watu hao wameuwawa kwa kupigwa na wananchi.
Vilevile kamanda Mponjoli amewataja waliouawa kuwa ni Paschal Charles (28) mkazi wa Bulengahasi na Pastori Magendo(30) ambaye yeye ni mkazi wa kata ya Ludete mtaa wa stooni mbali na hayo pia watu wawili wanashikiliwa kwa ajili ya upepelelezi zaidi kutokana na tukio hilo.
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoani Geita limetoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kwamba wale wote watakaobainika kuhusika katika tukio hilo sheria haitosita kuchukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya mauaji.
Post a Comment