WANANCHI WALILALAMIKIA JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA.
Lotson Mponjoli Kamanda wa polisi mkoa wa Geita.
Wananchi
mkoani Geita wameiomba serikali kudhibiti vitendo
vya rushwa nchini ambavyo vinapelekea kukosa haki zao za msingi
wanapohitaji kuzipata.
Wakizungumza
na Blog hii baadhi ya wananchi hao ambao wamelishutumu
jeshi la polisi kwa kuendelea kujihusisha
na vitendo hivyo ambavyo vimeonekana kuwabana
zaidi wananchi wenye kipato cha chini na kushindwa kupata haki zao.
Aidha
kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Lotson amekiri kuwepo kwa tuhuma hizo
huku akiwataka wananchi kuonyesha ushirikiano
hasa kwa vielelezo ili wanaojihusisha na vitendo hivyo wachukuliwe hatua za
kisheria.
Kwa
upande wake mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw.Thobias Ndaro amefafanua zaidi jinsi wanavyopambana na rushwa hasa kwa wananchi walioko vijijini na
kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano
pindi yatokeapo matukio hayo.
Kumsikia Kamanda akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo bonyeza HAPA
Post a Comment