WANAFUNZI WA CHUO CHA GLOBAL COMMUNITY MKOANI GEITA WALALAMIKIA CHUO HICHO KUKOSA USAJILI.
Chuo cha ukunga na uuguzi cha Grobal Community kilichopo Wilaya na Mkoani Geita kinalalamikiwa na wanafunzi wake kutokuwa na usajili.
Wakizungumza na storm habari kwa nyakati tofauti chuoni hapo,wamesema kuwa wamekuwa na wasi wasi na chuo hicho ni kutokana na mtaala wa masomo kutofautiana na vyuo vingine vya uuguzi pamoja na kutokupata ushirikiano pindi wanapokuwa katika masomo ya vitendo hususani katika hosptali na zahanati za serikali kwani wamekuwa wakiambiwa hawatambuliki.
Mmoja kati ya wanafunzi waliohitimu katika chuo hicho mwaka jana Rosemerry Jacktone,amesema kuwa anasikitishwa kwa kutokupatiwa cheti cha kumaliza tangu mwaka jana hali ambayo imeendelea kuwapa wasi wasi na kuwanyima fursa za kuangalia ajira kutokana na kutokuwa na cheti cha chuo.
Aidha Mkurugenzi wa chuo hicho, Bw.Denis Joel akizungumza na storm habari amesema kuwa chuo chake kimesajili wasiwasi wake anajua kuwa wale wanao kizonga chuo hicho ni baadhi ya watu wenye chuki na maendeleo.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu ,Mabera Ezekiel ameeleza kuwa kwa uhalisia uliopo katika chuo hicho ni kweli hakijasajiliwa kwani malalamiko ya wanafunzi yameshafika katika ofisi ya mganga mkuu muda mrefu na walikiomba chuo hicho kuhakikisha kuwa kinapeleka nyaraka ambayo inatambulika kuwa chuo hicho kimesajiliwa.
Post a Comment