MWALIMU AMBAKA MWANAFUNZI WAKE NA KUMSABABISHIA UJAUZITO GEITA.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Lotson Mponjoli
Jeshi la polisi
wilayani Bukombe mkoani Geita limemfikisha
mahakamani mwalimu Jackson Jilaa wa shule ya msingi Kakoyoyo
kata ya Bulega kwa kosa la kubaka na kumsababishia
ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16 aliyefaulu kujiunga
na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule ya sekondari Bulega.
Mbele ya hakimu mkazi
mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya wilayani hapo Gabriel
Kulwijira mwendesha mashitaka wa
polisi mkaguzi msaidizi Neema Naruke
ameieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa bila aibu na bila
kujali maadili ya utumishi alimbaka mwanafunzi
wake na kumsababishia ujauzito.
Amesema kuwa kitendo
alichokifanya mwalimu Jackson Jilala cha kumharibia
maisha mwanafunzi wake ambae alifauru mtihani wa darasa la saba ni kitendo cha udhalilishaji
na pia ni ukatili wa kijinsia.
Hata hivyo
mshtakiwa mwalimu
Jackson amekana shitaka na hakimu mfawidhi wa
mahakama ya wilaya Gabriel Kurwijila amemrudisha rumande
hadi hapo kesi itakapotajwa tena.
Post a Comment