MKUU WA WILAYA YA GEITA AWATAKA WANANCHI WA MKOA HUO KUMRUDIA MUNGU NA KUACHA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE
Mwimbaji Tumsifu(mwambie Farao)wakati akizunguka na baadhi ya watu waliojitokeza kwenye tamasha la pasaka jana katika ukumbi wa Desire.
Katika Tamasha hilo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo ameishukuru kampuni ya Msama Promotion na Mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa kuandaa tamasha hilo kwani hiyo ni fursa pekee ya baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita kumrudia Mungu na kutubu ili kuacha tabia mbaya inayoupaka matope mkoa huo kwa mauaji ya walemavu wa ngozi Albino pamoja na Vikongwe
Waimbaji mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo ambao ni Upendo Nkone, Bonny Mwaiteje, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Jesca BM, Jennifer Mgendi, Mwimbaji kutoka Zambia Ephraim Sekereti, Waimbaji kutoka Nchini Kenya Solomon Mukubwa , na Mtanzania Faustine Munishi pamoja naye Christopher Muhangila.
Matamasha hayo yataendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo na kesho litafanyika tamasha lingine kama hilo mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion chini ya mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa udhamini wa magazeti ya Dira, Dira TV na Dira FM na linafanyika kila mwaka katika kipindi cha sikukuu za Pasaka.

Post a Comment