Askari Polisi Anatafutwa Na Jeshi La Polisi Baada Ya Kugundulika Alijipatia Ajira Kwa Vyeti Vya Kugushi.
Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni Emanuel Nikolas Nyangoli mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya kutuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi aliamua kutoroka na hajulikani aliko.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema Askari Emanuel Nyangol amefanya kazi ndani ya jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 13 bila kujulikana kuwa ana vyeti vya kugushi,
Vielelezo vya kuonyesha jeshi la polisi lina taarifa kuwa uajiriwa wa askari huyo ni wakutatanisha ndio ulio mfanya atoroke baada ya kujua jeshi la polisi lina taka kumfungulia mashitaka
Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linawaomba wanchi ambao watakuwa na tarifa za Emanuel Nyangoli watoe tarifa kwa kituo chochote cha polisi au apige kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Nomber 0715 009 956.
Post a Comment