Natamani kuona Hisia akiimba kuhusu mazingira, maji, elimu – asema mama yake.
Mama mzazi wa muimbaji Hisia, Anna Mgwira amesema kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa kazi za mwanaye lakini wanatofautiana tu kwenye maudhui ya nyimbo zake.
Mama Hisia ambaye pia alikuwa mgombea urais kwenye uchaguzi uliopita kupitia ACT, amesema kuwa yeye sio shabiki wa nyimbo za mapenzi ambazo hata mwanaye ndio anazopenda zaidi kuimba.
“Kwanza hapo tunatofautiana mi na yeye kwamba anapenda kuimbaimba nyimbo za mapenzi sana mimi sionagi kitu kipya kwenye hayo mambo.” Alisema Mama Hisia kupitia Planet Bongo ya EA Radio. “yeye ananiambia aah labda wewe umezeeka (kicheko), lakini natamani sana aimbe mambo ya maisha zaidi, mapenzi sawa yapo lakini hakuna kipya sana kule.”
Baadhi ya nyimbo ambazo Hisia ameshaachia hadi sasa ni pamoja na ‘Gimme A Call’, ‘Mawazo’, ‘Keep You Warm’, ‘Just For You’ na zingine.
Mama Hisia ameongeza kuwa angependa kuona kijana wake anaimba zaidi nyimbo kuhusu mazingira, maji, elimu, ukimwi na mambo mengine kama hayo.

Post a Comment